SiasaUfaransa
Macron asaini sheria tata ya pensheni
15 Aprili 2023Matangazo
Chini ya sheria hiyo inayopingwa vikali na vyama vya wafanyakazi, umri wa kustaafu na kupata malipo ya uzeeni utapandishwa kutoka miaka 62 hadi 64.
Baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo yamezuuka maandamano makubwa na yenye vurugu katika miji mingi kote nchini Ufarnsa, ambapo watu 112 wameripotiwa kukamatwa na polisi mjini Paris pekee.
Waandamanaji wamezichoma moto baiskeli, skuta za umeme na mapipa ya taka katika mji huo mkuu, na katika mji wa Rennes, mlango wa kituo cha polisi na ofisi ya bunge vimeharibiwa katika ghasia hizo.
Awali vyama vya wafanyakazi vilikuwa vimemtaka Rais Emmanuel Macron kutoisaini sheria hiyo, na vimekataa mwaliko wake kwa mazungumzo Jumanne ijayo.