1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron ashinikizwa kujiuzulu kufuatia mgogoro wa kisiasa

8 Oktoba 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anakabiliwa na shinikizo kubwa, hata kutoka kwa washirika wake wa karibu, kutafuta suluhisho la haraka kwa mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini mwake.

Ujerumani Saarbrücken 2025 | Emmanuel Macron akizungumza kwenye sherehe kuu za umoja
Rais Emmanuel Macron atazungumza kwenye sherehe kuu za Siku ya Umoja wa Ujerumani katika Ukumbi wa Congress. Tarehe 3 Oktoba 2025Picha: Jean-Christophe Verhaegen/AFP/dpa/picture alliance

Katika hali ya kushangaza, Édouard Philippe, Waziri Mkuu wa kwanza wa Macron, amemtaka rais ajiuzulu kwa maslahi ya taifa, akisema kuwa hali ya sasa ya kisiasa inadhuru Ufaransa. Philippe alipendekeza uchaguzi wa mapema wa urais mara tu baada ya bajeti ya 2026 kupitishwa. Hali hii imechochewa zaidi na kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Sébastien Lecornu, aliyeteuliwa chini ya mwezi mmoja uliopita, na ambaye sasa anakuwa Waziri Mkuu wa saba kuondoka madarakani chini ya utawala wa Macron tangu 2017.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW