1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron atangaza mkutano wa kuisaidia Lebanon

17 Januari 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kwamba Paris itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa ujenzi mpya katika wiki zijazo.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Lewis Joly/AP Photo/picture alliance

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kwamba Paris itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa ujenzi mpya katika wiki zijazo  baada ya vita kati ya wanamgambo wa Hezbollah na Israel.

Soma: Rais Macron awasili nchini Lebanon kuonyesha uungwaji mkono

Macron amesema baada ya Rais wa Lebanon, Joseph Aoun kwenda Paris wiki chache zijazo, wataandaa mkutano wa kimataifa wa kukusanya fedha kwa ajili ya ujenzi mpya.

Ameiambia jumuiya ya kimataifa kujiandaa kutoa msaada mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. 

Waziri Mkuu mpya wa Lebanon Nawaf Salam, anakabiliwa na kazi kubwa ya kuunda serikali itakayosimamia ujenzi huo mpya baada ya kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hezbollah.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW