Macron atangaza rasmi mwisho wa jeshi lake nchini Mali
10 Novemba 2022Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza rasmi Jumatano kuwa ujumbe wa kupambana na ugaidi nchini Mali umefikia tamati baada ya wanajeshi wa mwisho wa ujumbe wa Ufaransa unaojulikana kama Barkhane kuondoka katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi mwezi Agosti.
Mali yaituhumu Ufaransa na kutishia kujihami
Baada ya kuendesha harakati hizo kwa miaka tisa, Macron amesema akiwa katika mji wa kusini mwa Ufaransa wa Toulon kuwa Ufaransa itaendeleza ushiriki wake katika Sahel lakini itabadilisha mkakati wake na kujikita katika operesheni za muda na za ushirikiano. Kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa nchini Mali kulitokana na mvutano baina ya Paris na utawala wa kijeshi wa Bamako.
Chanzo cha mzozo wa Mali na mshirika wake Ufaransa
Takriban wanajeshi 3,000 wa Ufaransa bado wako nchini Niger, Chad na Burkina Faso ili kusaidia kupambana na makundi kadhaa yenye silaha katika eneo la Sahel, ambayo baadhi yamekuwa na mafungamano na makundi ya kigaidi kama linalojiita Dola la Kiislamu IS au kundi al-Qaeda.