1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron atoa wito wa utulivu kuhusu mpango wa pensheni

20 Machi 2023

Rais Macron wa Ufaransa amesema anatumai kuwa mpango wake wa mageuzi ya pensheni unaopingwa vikali, ambao ulilazimishwa kupita bungeni bila kupigiwa kura, huenda ukakamilisha kile alichokiita safari yake ya kidemokrasia.

Frankreich Rentenrefrom l Misstrauensvotum gegen Macron
Picha: Ludovic Marin/Pool via REUTERS

Sheria hiyo tata, ambayo imesababisha miezi kadhaa ya upinzani na maandamano, itaidhinishwa bungeni leo isipokuwa kama moja kati ya miswada miwili ya kutokuwa na imani na serikali utapitishwa.

Katika taarifa hiyo, Macron amesema jana kuwa baada ya miezi ya mashauriano ya kisiasa na kijamii, na zaidi ya masaa 170 ya mjadala ambao ulipelekea kura rasmi ya maelewano kati ya mabunge yote mawili, sheria hiyo sasa inaweza kufikia mwisho wa safari yake ya kidemokrasia na heshima kwa wote.

Soma pia: Ufaransa yakabiliwa na maandamano zaidi kuhusu sheria ya pensheni

Kama sheria hiyo itaidhinishwa, mageuzi hayo ya Macron yataongeza umri wa kisheria wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64 pamoja na kuongeza idadi ya miaka ambayo watu lazima wachangie kwenye mfumo huo ili kupokea pensheni kamili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW