1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron atuma ujumbe kwa Trump kutaka kuandaa mkutano wa G7

20 Januari 2026

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametuma "ujumbe wa faragha" kwa mwenzake wa Marekani Donald Trump, akitaka kuandaa mkutano wa kilele wa G7 mjini Paris siku ya Alhamisi.

Ubelgiji Brüssel 2025 | Emmanuel Macron akihudhuria mkutano wa viongozi wa Eu mjini Brussels mnamo Desemba 18 na 19, 2025
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: Nicolas Tucat/AFP

Macron amesema Ukraine, Urusi, Denmark na Syria pia zinaweza kualikiwa pembezoni mwa mkutano huo.

Haya yamethibitishwa na vyanzo vya karibu na rais huyo.

Katika ujumbe huo, Macron amemwambia Trump kwamba wako pamoja katika suala la Syria na kwamba wanaweza kufanya mambo makubwa nchini Iran.

Ameongeza kusema haelewi anachokifanya Trump kuhusu kisiwa cha Greenland.

Trump pia alichapisha ujumbe huu kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth.

Uhusiano wa Trump na Macron ulizidi kudidimia jana wakati rais huyo wa Marekani alipotishia kutoza asilimia 200 ya ushuru kwa mvinyo wa Ufaransa kutokana na nia ya nchi hiyo ya kukataa mwaliko wa kujiunga na "Bodi yake ya Amani".

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW