Macron autuhumu upinzani "kuihujumu" jamhuri
6 Desemba 2024Matangazo
Kwenye hotuba yake kwa taifa jioni ya jana, Macron alidai kwamba serikali yake iliporomoka kwa sababu ya wabunge wa mrengo mkali wa kulia na kushoto kuungana kuunda umoja wa kuidhuru nchi.
Soma zaidi: Macron aapa kusalia madarakani baada ya serikali kuporomoka
Ingawa alikiri makosa yake mwenyewe yaliyopelekea kuvunjika kwa serikali ya Waziri Mkuu Michel Barnier, Macron alisema asingelibeba dhamana kwa makosa ya wengine, hasa wabunge walioamuwa kwa makusudi kuipinga bajeti na serikali siku chache kabla ya mapumziko ya Krismasi.
Kambi ya mrengo wa kushoto na ile ya mrengo wa kulia inayoongozwa na Marine Le Pen, siku ya Jumatano ziliungana bungeni kuiangusha serikali ya Barnier iliyodumu madarakani kwa miezi mitatu tu.