1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron awasili Kenya kutokea Misri

11 Mei 2026

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana na mwenzake wa Kenya William Ruto mjini Nairobi.

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akiwa na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sissi
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akiwa na mwenzake wa Misri Abdel Fattah al-Sissi Picha: Ludovic Marin/AFP

Hii ni kama sehemu ya ziara yake barani Afrika inayolenga kufufua mahusiano ya Ufaransa na bara hilo baada ya miaka kadhaa ya kuvurugika kwa mahusiano hayo.

Katika ziara hiyo Macron atahudhuria mkutano wa kilele wa siku mbili utakaoanza leo Jumatatu.

Mkutano huo utawaleta pamoja viongozi wa Afrika na wakurugenziwa kibiashara, mwaka mmoja kabla muhula wake kufikia mwisho.

Afisi ya Macron imesema mkutano huo wa kilele utajikita katika ustawi wa kiuchumi na uwekezaji miongoni mwa masuala mengine. Macron amewasili Kenya kutoka Misri na katika ziara hiyo anatarajiwa pia kuelekea Ethiopia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW