Macron kumtaja waziri mkuu mpya wa Ufaransa
9 Oktoba 2025
Matangazo
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atamteua waziri mkuu mpya katika kipindi cha saa 48 zijazo.
Hayo yamesemwa na ofisi yake Jumatano, baada ya kujiuzulu kwa waziri mkuu anayeondoka Sebastien Lecornu kuashiria nchi hiyo kuingia katika mzozo wa kisiasa.
Awali Lecornu aliiambia televisheni ya Ufaransa katika mahojiano kwamba alitarajia waziri mkuu mpya kutajwa -- badala ya uchaguzi wa mapema wa wabunge kuitishwa au Macron kujiuzulu -- katika jitihada za kuutatua ufumbuzi mgogoro huo.
Jumatatu wiki hii Macron alimpa Lecornu hadi Jumatano jioni kutafuta njia ya kutoka kwa kipindi kigumu cha miezi kadhaa ya msuguano juu ya bajeti ya kubana matumizi.
Lecornu alijiuzulu mapema Jumatatu baada ya kuwa madarakani kwa chini ya mwezi mmoja.