1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron kutembelea Mayotte kilichoharibiwa na Kimbunga Chido

17 Desemba 2024

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amepanga kukitembelea kisiwa cha Bahari ya Hindi cha Mayotte kufuatia Kimbunga Chido kupiga eneo hilo na kusababisha maafa makubwa.

Frankreich Paris 2024 | Macron leitet Krisensitzung zu Folgen des Zyklons Chido auf Mayotte
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaongoza mkutano wa mgogoro unaohusu hali katika eneo la Bahari ya Hindi la Ufaransa la kisiwa cha Mayotte baada ya kimbunga Chido Desemba 16, 2024.Picha: Ludovic Marin/REUTERS

Kupitia ukurasa wake wa X, Macron alisema atakitembelea kisiwa hicho ndani ya siku kadhaa zijazo, kuwaunga mkono raia wake, maafisa na mashirika ya kutoa huduma muhimu. Macron pia alisema anapanga kutangaza kipindi cha maombolezo cha kitaifa. Hadi sasa serikali imetangaza vifo vya watu 21 huku zaidi ya watu 1,400 kujeruhiwa vibaya  kutokana na kimbunga hicho, kilichopiga eneo hilo lililochini ya Ufaransa na kusababisha uharibifu wa majengo, miundombinu ya nishati na mawasiliano Wakoaji wanaendelea na juhudi za kuwafuta manusura na kurejesha huduma muhimu huko.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW