1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron kutumia kifungu cha katiba kuptisha mfumo wa pensheni

16 Machi 2023

Serikali ya Ufaransa inapanga kutumia mamlaka maalum ya kikatiba kuidhinisha mageuzi katika mfumo wa pensheni wa nchi hiyo bila ya muswaada huo kupigiwa kura bungeni.

Frankreich Paris | Parlament zu Rentenreform
Picha: PASCAL ROSSIGNOL/REUTERS

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameamua kulazimisha kuuidhinisha mpango wake wa mageuzi ya pensheni bila kuitisha kura bungeni.

Maandamano mapya kuhusu muswada wa pensheni Ufaransa

Vyanzo kadhaa vilivyo karibu na ofisi ya rais vimeliambia shirika la habari la AFP kwamba kiongozi huyo atatumia uwezo wa kikatiba unaoiwezesha serikali kuwapiku wabunge.

Rais Macron amechagua kukitumia kifungu cha 49.3 cha katiba ya Ufaransa baada ya mikutano kadhaa na viongozi wakuu, akiwemo Waziri Mkuu Elisabeth Borne, baada ya kubaini kwamba hakukuwepo na wabunge wengi wa kupitisha mageuzi hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW