SiasaAsia
Macron na Modi wafanya mazungumzo New Delhi
17 Februari 2026
Matangazo
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa India Narendra Modi yaliyolenga kuimarisha mahusiano ya kiuchumi na kimkakati, wakati mataifa hayo mawili yakitafuta ushirikiano wa karibu zaidi kufuatia hali ya mashaka inayoikabili dunia pamoja na kubadilika kwa mirengo ya siasa za kikanda.
Mazungungu hayo yamefanyika mjini New Delhi yakijikita zaidi katika kukuza ushirikiano kwenye masuala ya ulinzi, biashara, teknolojia na nishati huku Ufaransa ikijinadi kama mmoja wa washirika muhimu wa kutegemewa na India barani Ulaya.
Viongozi hao wawili pia wamezinduwa kwa pamoja kiwanda cha kukamilisha uundaji wa helikopta chapa H125 katika jimbo la Karnataka Kusini mwa India.