1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUfaransa

Macron: Ufaransa kuipatia Ukraine makombora ziada ya masafa

17 Januari 2024

Ufaransa imetangaza itaipatia Ukraine shehena mpya ya makombora ya masafa yapatayo 40 pamoja na mamia ya mabomu kuliongezea nguvu jeshi la nchi hiyo kupambana na vikosi vya Urusi.

Mfano wa kombora la SCALP
Makombora aina ya SCALP yana uwezo wa kusafiri umbali mrefuPicha: Photoshot/picture alliance

Makombora hayo ya nyongeza aina ya SCALP yana uwezo wa kushambulia kwa umbali wa hadi maeneo ya mashariki mwa Ukraine yaliyonyakuliwa na Urusi.

Tangazo la kutumwa makombora hayo nchini Ukraine limetolewa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron usiku wa kuamkia leo akisema kipaumbele cha Ulaya ni lazima kiwe "kuizuia Urusi kushinda" vita vya Ukraine.

Macron amesema iwapo Urusi itashinda vita hivyo hilo litamaanisha "kwamba Ulaya imeridhia kutoheshimiwa kwa sheria za kimataifa."

Mbali ya msaada huo, Macron pia ametangaza kuwa atafanya ziara nyingine nchini Ukraine mnamo mwezi Februari