1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Macron: Ulinzi wa kujitegemea Ulaya haufai

13 Julai 2026

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amezionya nchi za Ulaya dhidi ya kila mmoja kusimamia kivyake sera yake ya ulinzi wa taifa.

Frankreich Paris 2026 | Emmanuel Macron bei Ansprache an die Streitkräfte vor dem Nationalfeiertag
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Picha: Thomas Padilla/REUTERS

Kauli hiyo inajiri wakati serikali za mataifa hayo zikiongeza bajeti zao za kijeshi kutokana na kitisho cha Urusi na shinikizo la  Marekani kutaka nchi hizo kuongeza bajeti zao za ulinzi.

Hotuba ya Macron katika ufunguzi wa mkutano wa washirika wa Ukraine unaojulikana kama  "muungano wa walio tayari" unaofanyika mjini Paris, imekuja mwezi mmoja baada ya kuvunjika kwa mradi wa pamoja wa Ufaransa na Ujerumani wa kutengeneza ndege za  kivita kufuatia miezi kadhaa ya mkwamo kati ya kampuni za ulinzi.

Hali hiyo imeonyesha ushindani wa kiviwanda unaoweza kudhoofisha juhudi za Ulaya za kujiimarisha kijeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW