1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada muhimu kabisa inayotiliwa uzito na magazeti mengi ya Ujerumani hii leo ni kule kujiuzulu Kansela wa Ujerumani uwanachama wa chama-tawala SPD

Manasseh Rukungu9 Februari 2004
Gazeti mashuhuri la kusini mwa Ujerumani, FRANKFURTER RUNDSCHAU, kuhusu mada hjii linaandika: Vitisho vya Kansela vya uwezekano wa kujiuzulu kwake wadhifa huu wa mwenyekiri wa chama tawala SPD, vimeshakamilika. Sasa kile kinachobaki, ni kama halikadhalika atalifanyia mageuzi baraza lake la mawaziri. Hapana shaka Kansela amechukua hatua hii, pindi kuokoa sifa ya chama inayozidi kudidimia, ameamua kushikilia mkondo wa mageuzi ya siasa za huduma za kijamii. Lakini mfuasi wake mteule mwenyekiti wa chama Franz Münterfering, kuna shakashaka kama atafanikiwa kuweka hali ya busara zaidi, isipokuwa kuendelea kuwa mwaminifu katika muongozo wa chama. Gazeti mashuhuri la biashara, FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND, nalo linakisia: Kujiuzulu kwa Kansela Gerhard Schröder kama mwenyekiti wa SPD kunakipatia chama kizima muda wa kuvuta pumzi. Kwa Kansela Schröder na hata kwa Ujerumani binafsi, hatua yake ya kuweka jopo la nyadhifa mbili katika uongozi wa chama, inaweza ikawa ya hatari. Hii ilikuwa ni hatua ya mwisho ya Kansela kujiokoa na yale yaliyokuwa yakimkabili wakati uliopita. Jaribio ambalo huenda likamuokoa Kansela Schröder mnamo kipindi cha miaka mitatu iliyobaki hadi kufanyika uchaguzi mkuu ujao. Jaribio ambalo limampunguzia nafasi ya kuendeleza mkondo wa mageuzi ya " Angeda 2010" hadi ufikapo mwaka huo wa uchaguzi mkuu wa 2006. Nalo gazeti mashuhuri la mji mkuu Berlin, BERLINER ZEITUNG, katika uhariri wake kuhusu mada hii linakisia: Kwa haua ya Kansela kujiuzulu wadhifa huu, zinatengana hali mbili, ambazo hazikuwahi kuwa pamoja. Kujitenga kwa Kansela na wadhifa huu wa mwenyekiti wa chama, hapana shaka kunatokana na yale yaliyotangulia mnamo miaka iliyopita. Franz Münterfering ni mtu anayefaa kushikilia wadhida huu, lakini katika wakati usiofaa. Kinyume chake, ni kosa kuchaguliwa Klaus Uwe Benneter kuwa ni katibu-mkuu wake. Mada hii inazingatiwa na gazeti mashuhuri la hapa jijini Bonn, GENERAL-ANZEIGER, linaposema: Sasa chama-tawala cha SPD, kinakabiliwa na kitisho cha kushindwa katika chaguzi. Ndio maana Franz Müntedrfering ameteuliwa ni mwenyekiti, pindi kuokoa sifa ya chama, hali ambayo inazusha hangaiko kubwa miongoni mwa wanachama. Kama katibu mkuu mpya Klaus Uwe Benneter, atafanikiwa kumsaidia katika jukumu hili, inabidi kusubiriwa., kwa sababu Kansela amelazimika kumteua mwenyekiti mpya wa chama. Labda huu utakuwa mwanzo mpya? Au utakuwa mwanzo wa mwisho wa chama hiki mashuhuri cha umma? Gazeti mashuhuri kibiashara la mji wa magharibi wa Düsseldorf, HANDELSBLATT, nalo linasema: Franz Münterfering hapotezi wakati. Mara tu baada yakuteuliwa, ameshaapa kushikia usukani uongozi wa chama kulingana na mpango wa mageuzi wa Kansela. Mteule mwenyekiti Münterfering, alijifunza mengi hasa mnamo mwaka uliopita wa kuwa wakili wa kuwakilisha mageuzi hayo. Hawezi kusalimu amri, kwa sababu hatua kama hii pia ingedhoofisha haiba yake. Tunakamilisha mada hii kwa kutazama yale yanayohaririwa na gazeti lingine mashuhuri la kusini mwa Ujwerumani, SÜDDEUTSCHE ZEITUNG, linapoandika: Franz Münterfering mwenye umri wa miaka 64, atakuwa ni mwenyekiti wa mpito tu wa chama cha SPD. Lakini muda atakavyoweza kusalia madarakani, yote yatategemea hatima mpya ya Gerhard Schröder, kwani Schröder sio kansela wa Münterfering, bali Münterfering atakuwa mwenyekiti mpya wa chama wa Schröder. Kwa maneno mengine, wote wawili ni kama mapacha wasiotenganika wa kutumikia muongozo wa chama hiki mashuhuri cha umma SPD.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW