Mada za Migogoro, tabianchi na AI kuugubika mkutano wa Davos
15 Januari 2024Mkutano wa Jukwaa la Uchumi duniani unafunguliwa leo kwenye mji wa Davos nchini Uswisi, ambapo unatarajiwa kugubikwa na masuala ya ongezeko la joto duniani, mgogoro wa mashariki ya kati, uchumi wa ulimwengu na ulinzi wa Ukraine dhidi ya Urusi.
Zaidi ya wakuu 60 wa nchi na serikali, akiwemo Rais Isaac Herzog na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wanaelekea Davos kwa ajili ya mazungumzo.
Watakuwa miongoni mwa washiriki 2,800, ambao watajumuisha wasomi, wasanii na viongozi wa mashariki ya kimataifa.
Ikulu ya Urusi imesema mazungumzo kuhusu mapendekezo ya amani katika magogoro wa Ukraine hayatafanikiwa kwasababu nchi hiyo haitoshiki.
Mkutano wa Davos unalenga ushirikiano wa amani na usalama, au maboresho ya kubadilisha hali ya maisha katika huduma za afya, na pia ni jukwaa la watoa maamuzi katika sekta mbalimbali kuwasiliana. Mkutano huo utafunguliwa rasmi kesho na kukamilika Ijumaa wiki hii.