1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMadagascar

Madagascar yafanya uchaguzi wa rais uliosusiwa na upinzani

16 Novemba 2023

Watu nchini Madagascar wamepiga kura leo katika uchaguzi wa rais ambao umesusiwa na wagombea wengi wa upinzani kufuatia wiki kadhaa za vurugu na kesi za mahakamani.

Andry Rajoelina | Rais wa Madagascar
Rais Andry Rajoelina anawania muhula mwingine madarakani Picha: Abd Rabbo Ammar/ABACA/IMAGO

Katika mji mkuu Antananarivo, ambako amri ya kutokuwa nje usiku ilikamilika saa mbili kabla ya vituo vya kupigia kura kufunguliwa, watu wengi waliitikia miito iliyotolowa na wagombea 10 ya kuwataka wajiepushe na shughuli hiyo.

Viongozi wa upinzani na mashirika ya kiraia pia yalikuwa yametoa wito wa kuahirishwa uchaguzi huo.

Akizungumza baada ya kupiga kura yake mapema leo, Rais Andry Rajoelina aliwahimiza watu kujitokeza na kushiriki katika zoezi hilo akisema kuwa njia pekee ya demokrasia ni uchaguzi.

Watu milioni 11 wamesajiliwa kupiga kura katika taifa hilo la kisiwa cha Bahari Hindi chenye jumla ya watu milioni 30.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW