1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madai 290 unyanyasaji wa kingono kanisani yawasilishwa

12 Aprili 2022

Kamati ya viongozi wa kanisa inayochunguza historia ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto katika Kanisa Katoliki Ureno limesema limepokea taarifa za mashahidi kutoka kwa waathirika 290 katika miezi mitatu ya mwanzo.

UK London Sex Skandal an Schulen
Picha: Kerry Davies/SOLO Syndication/picture alliance

Taarifa hizo za ushahidi zilizowasilishwa katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ziliwahusu watoto pia hadi wenye umri wa miaka miwili.

Zaidi ya nusu ya kesi zilizoripotiwa zinaonyesha kuna waathiriwa wengi zaidi wanaohusika, alisema Pedro Strecht, daktari wa magonjwa ya akili ambaye pia ni kiongozi wa Kamati Huru ya Utafiti wa Unyanyasaji wa Watoto Kanisani.

soma zaidi:Unyanyasaji wa kingono Ufaransa aibu kwa kanisa asema Papa

Kamati hiyo ya watu sita, ambayo inajumuisha madaktari wa magonjwa ya akili, jaji mstaafu wa mahakama ya juu na mwanaharakati wa ustawi wa jamii, ilianza kazi yake mwezi Januari kama agizo kutoka Baraza la Maaskofu wa Ureno. Inaahidi kuficha jina la yeyote anayejitokeza na kutaka kutotambuliwa.

Strecht alisema kamati hiyo imekutana na ishara ambazo maafisa wa kanisa, wakiwemo maaskofu wa sasa ambao hakuwataja, walitafuta namna ya kuficha unyanyasaji huo.``Mara nyingi mnyanyasaji alikuwa anahamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine, ikiwa atajulikana kwa wakati huo,'' Alisema Strecht.

 

Kamati:Maaskofu wote wafanyiwe mahojiano

Kamati hiyo imewataka maaskofu wote 21 wa Ureno kufanyiwa mahojiano ili kujadili kazi yake. Ni maaskofu 12 tu ndio wamekubali kufanya mkutano na watano hawajajibu.

utulivu wa kanisa ndaniPicha: John Roark/Athens Banner-Herald/AP/picture alliance

  Mwanasosholojia na mjumbe wa kamati hiyo, Anna Nunes Almeida wa Chuo Kikuu cha Lisbon aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa madai yaliyoorodheshwa kufikia sasa yanahusiana na unyanyasaji dhidi ya watoto wenye umri wa kati ya miaka miwili na 17.

Kulikuwa na aina mbalimbali za madai ya unyanyasaji, alisema, ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia.

  Soma zaidi:Watoto 330,000 wamenyanyaswa kingono katika Kanisa Katoliki

Matukio hayo yanadaiwa kutokea wakati watoto wakifanya huduma za kanisa, wakiwa kwenye vikundi kama vile vikundi vya masomo ya kateksimu. Wengi wa walioathiriwa zaidi ni watoto wa kiume.

Jaji mstaafu Alvaro Laborinho Lucio alisema kamati hiyo imewasilisha Kesi 16 kwenye ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma.

``Kwa miaka mingi kumekuwa na unyanyasaji wa kingono uliofanywa ndani ya Kanisa Katoliki la Ureno,'' alismea Laborinho Lucio.