1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Madaktari: Afya ya Biden ni njema

Daniel Gakuba
17 Februari 2023

Madaktari wametangaza kwamba rais Joe Biden wa Marekani yuko salama salimini baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya. Akiwa na miaka 80 Biden anakuwa rais mkongwe zaidi miongoni mwa marais waliowahi kuiongoza Marekani.

USA Washington Weißes Haus | Joe Biden, Präsident
Picha: Kevin Lamarque/REUTERS

Majibu ya vipimo vya kitabibu alivyofanyiwa rais wa Marekani Joe Biden yameonyesha kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 ni buheri wa afya na anaweza kuyatekeleza vyema majukumu yake. Majibu hayo ya baada ya uchunguzi wa masaa matatu yalisubiriwa kwa shauku kwa kuzingatia azma ya rais huyo kugombea muhula wa pili katika uchaguzi wa mwakani. Biden alichukuliwa vipimo katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed iliyoko Bethesda, Maryland ambapo matatizo madogo madogo yamegunduliwa lakini hakukutwa na madhara ya muda mrefu yatokanayo na maambukizi ya UVIKO ambayo yalimsibu mara mbili. Katika barua iliyochapishwa katika tovuti ya Ikulu ya Marekani, The White House,  Daktari wa Rais Biden, Kevin O'Connor amesema rais huyo ana afya njema na nguvu za kutosha kuendesha majukumu yake kama kiongozi wa serikali na amiri mkuu wa jeshi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW