1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Maelfu huenda wakapoteza maisha katika hospitali, Gaza

15 Oktoba 2023

Madaktari kwenye Ukanda wa Gaza wametahadharisha kwamba huenda maelfu ya watu wakapoteza maisha ikiwa hospitali zilizojaa watu waliojeruhiwa zitaishiwa mafuta na mahitaji mengine muhimu.

Madaktari wawatibu majeruhi wa shambulizi la Israel dhidi ya hospitali ya Nasser mjini Khan Yunis katika ukanda wa Gaza mnamo Oktoba 13, 203
Madaktari wawatibu majeruhi wa shambulizi la Israel katika ukanda wa GazaPicha: Abed Zagout/Anadolu/picture alliance

Daktari huyo mkuu katika hospitali ya Ukanda wa Gaza ameeleza kuwa wagonjwa 35 wamelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na wanategemea mashine za kuwasaidia kupumua na wengine 60 wanaofanyiwa huduma ya kusafishwa figo na kwamba mafuta yatakapoisha, watalazimika kuzima mkitambo na hivyo kukatizsha huduma hizo.

Soma pia:Wapalestina 2,220 wameuawa katika mashambulizi ya Israel ukanda wa Gaza

Wakati huohuo raia wanahangaika kutafuta chakula, maji na mahala salama wakati ambapo Israel inajiandaa kufanya operesheni ya ardhini kujibu mashambulio ya Hamas ya wiki iliyopita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW