Madaktari wakataa pendekezo la kusitisha mgomo Kenya
4 Aprili 2024Matangazo
Kiasi wanachama 7,000 wa chama cha madaktari (KMPDU) walianza mgomo katikati mwa mwezi Machi kudai mishahara bora na mazingira mazuri zaidi ya kazi.
Mahakama inayoshughulikia masuala ya ajira na wafanyakazi iliusitisha mgomo huo mwezi uliopita na siku ya Jumatano (Aprili 3) ikaamuru mashauriano yanayoendelea yatoe suluhisho katika kipindi cha siku 14.
Soma zaidi: Madaktari Kenya wakataa pendekezo la serikali kusitisha mgomo
Umauzi huo ulitolewa siku moja baada ya serikali kusema itayatimiza madai ya madaktari, yakiwemo malimbikizo ya mishahara na kuwaajiri madaktari wapya kwa mikataba ya kudumu.