1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMisri

Madbouly aahidi kuzuia mzozo kati ya Hezbollah na Israel

19 Desemba 2025

Waziri Mkuu wa Misri Mustafa Madbouly amesema kuwa nchi yake inafanya kila iwezalo kuzuia kuongezeka kwa mvutano kati ya Lebanon na Israel, hususan kuhusu mchakato wa kuwapokonya silaha wanamgambo wa Hezbollah.

Lebanon | Beirut 2025 | Haytham Tabtabai
Wafuasi wa Hezbollah wakibeba majeneza ya Mkuu wa Majeshi wa Hezbollah Haytham Tababai na wapiganaji wawili wa Hezbollah waliouawa katika shambulio la anga la Israel Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salim, Madbouly amewaambia waandishi wa habari kwamba Misri itaendelea kuimarisha juhudi za kuhakikisha Lebanon inabaki mbali na mzozo na jirani yake Israel.

Ziara ya Madbouly mjini Beirut imefanyika wakati kamati inayosimamia utekelezaji wa usitishaji mapigano uliofadhiliwa na Marekani - uliomaliza vita kati ya Israel na Hezbollah mwaka mmoja uliopita - ilikuwa ikifanya mkutano mwingine leo.

Misri ambayo ilisaini mkataba wa amani na Israel mwaka 1979, imekuwa ikifanya kazi kwa miezi kadhaa kupunguza mvutano wa kikanda.

Ziara ya Waziri Mkuu Madbouly inafuatia safari kama hizo zilizofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri pamoja na mkuu wa idara ya ujasusi.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW