1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madereva wa treni wa Ujerumani watishia kugoma januari

21 Desemba 2007

BERLIN:

Tisho la kufanyika mgomo wa madereva wa treni hapa Ujerumani mwezi ujao,umepelekea waziri wa usafiri wa Ujerumani- Wolfgang Tiefensee- kutaka kukutana haraka na wakuu wa reli nchini pamoja na wakuu wa vyama vya wafanya kazi. Mkuu wa chama cha madereva hao treni hapa Ujeruamni- Manfred Schell amesema kuwa atahudhuria mkutano huo.Mapema wiki hii,chama cha madereva hao kilisema kuwa kitaendelea na mgomo wake kuanzia Januari 7 ambao kiliuanza Julai hadi kinakapofanikiwa kupata ilichokiita malipo yanayotosheleza.Madereva wa Treni wanataka nyongeza ya asili mia 6 Unusu ya mshahara wao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW