Madereva wakubaliana na shirika la reli kuhusu mishahara
26 Machi 2024Hatua hiyo imeumaliza mgogoro wa kikazi ambao ulisababisha migomo kadhaa na hata kufunguliwa kwa kesi mahakamani. DGL imesema kuwa maelezo zaidi yatatolewa katika kikao cha waandishi habari mjini Berlin Jumanne. Deutsche Bahn pia imesema itafanya mkutano na waandishi habari Jumanne mjini Berlin kuzungumzia hali ya sasa ya mazungumzo ya mishahara.
Soma pia: Madereva wa treni wa Ujerumani wagoma tena leo
Duru sita za mazungumzo, msururu wa migomo, mazungumzo yaliyoshindwa na kesi za mahakamani viliigubika hali hiyo ya kutoelewana katika miezi ya karibuni.
Migogoro mingine kadhaa ya kikazi, hasa inayohusisha viwanja vya ndege Ujerumani na shirika kubwa kabisa la ndege Ujerumani - Lufthansa, bado haijatatuliwa. Migogoro hiyo kwa pamoja ilivuruga shughuli za usafiri wa umma nchini Ujerumani katika wiki za karibuni hatua iliyosababisha ukosoaji mkubwa wa kisiasa na umma.