1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madhehebu ya pentecosta Lagos,Nigeria

10 Septemba 2007

Madhehebu ya pentecosta yametia fora katika jiji la Lagos la Nigeria. Makanisa ya mitaani yamesheheni waumini ,lakini nini kinachowavutia ?

Mji wa Lagos wa Nigeria,sio tu ni shina la biashara la nchi yenye wakaazi wengi kabisa barani Afrika,bali pia umegeuka ngome ya kuhubiri dini ya kikiristu na ya umisionari.

Lagos, imesheheni tangu vikanisa vidogo vya madhehebu za pentecosta-au walokole,hadi shina la ufundi wa kimambo-leo (high-Tech)katika maswali ya dini ya kikristu.Ni mji ulioenea makathederali.

Mafanikio makubwa ya makanisa haya ya madhehebu ya pentecosta yaliochomoza kwa wingi mitaani mjini Lagos,yameanza pia kuyagubika makanisa ya desturi ya kikristu yenye mizizi yake barani Afrika.

Yanapiga muziki wa mitindo ya kimambo-leo,yanahubiri kwa vikuza sauti majiani yakinadi vita dhindi ya mashetani na mazimwi na kuahidi matibabu ya miujiza.Yote haya yanayapatia makanisa haya waumini wapya.

“ Wakati wa sherehe ya Fingsten,sisi waumini wa Yesu Kristu tunajiwa na “Roho mtakatifu” kutoka mbinguni na tunabatizwa kwa jina la yesu.”

Kama muumini huyu anaekwenda katika kanisa la madhehebu ya ‘Pentecosta”,mamia ya waumini wengine kila jumapili nao wataka nao kubarikiwa na Roho mtakatifu.Kwani siku hii humiminika waumini hawa katika makanisa yasiohesabika tangu yale madogo hata makubwamjini humu.

Miongoni mwa wale waliofanikiwa mno wamejenga kathederali katika barabara inayoelekea mjini Ibadan,likikidhi waumini hadi alfu 10.Barabara hii kuu ya kidini-Religion Highway-imeshageuka ulimwenguni kuwa alama ya kutambulisha ufanisi unaoletwa n a makanisa kama haya yanayovutia barani Afrika.

Kile ambacho kinachowavutia watu na makanisa ya madhehebu hizi, ni matumaini ya kujikomboa kutoka umasikini na magonjwa huku huku duniani na sio akhera.Wakati makanisa ya desturi tunayoyafahamu mara nyingi huahidi jaza ya mema baada ya kifo,makanisa haya ya “Pentecosta” huahidi jaza moja kwa moja katika uhayi huu kutoka baraka za Mungu.

Mhandisi Ejiah Ndifon kwa shabaha hiyo ameanzisha kanisa lake aliloliita “Royal Kingdom Citizen International “.Na tangu wakati huo, amekuwa akijiita ni “mtume”. Anaelezea ujumbe wake namna hivi :

“kuna wanadamu wengi ambao maisha yao yangeweza kuongoka mno,lakini hawakuweza kuongoka, kwavile hakuna mtu wakuwasaidia kutekeleza matarajio yao.

Kanisa la Royal Kingdom Citizen kwahivyo linawaongoza ,linawaleta binadamu hao na maisha yao yende sambamba na yale mema anayoamrisha Mungu.Shabaha hapa ni kuwawezesha kile kipao walichopewa na Mwenye Enzi Mungu wakifikie.”

Kwa njia hii waumini hawa wanaarifiwa kuwa Roho mtakatifu aweza kugeuza hatima zao kufuata mkondo ulio mwema.Kwani, maradhi na ukosefu wa ufanisi, huwakumba wale wasiojikinga na maovu na wasiofuata maamrisho ya Mungu.Katika vita hivi

Dhidi ya maovu makubwa ndipo ulipo msingi wa mafanikio ya makanisa ya aina hii Pfingst-asema Bw.Erhard Kamphausen,kiongozi wa miaka mingi wa Kitovu cha umisionari cha chuo kikuu cha Hamburg:

“Mila za jadi za kiafrika ambazo hazikuweza kujumuishwa ndani ya ukristu,huingizwa kamili katika makanisa haya yaliochomoza.

Hivyo ni kusema itikadi za ucahwi na mazingaombo ambazo zimekataliwa na makanisa ya kawaida yaliopo,zinakubaliwa na kuingizwa katika shughuli za makanisa haya ya Pantekosta.Uchawi na mazingaombo ni ukweli wa mambo ambao mtu apaswa kupamban nao kwa nguvu zake za kuushinda.”

Kutumia nguvu hizi dhidi ya maovu waumini hawa wanajionea wakati wa ibada zao.Waumini wake kwa waume hutoa ushahidi kwamba Roho mtakatifu amewasaidia.