MADRID : Malkia wa baadae nchini Uhispania ajifunguwa mtoto wa kike
31 Oktoba 2005Matangazo
Malkia wa baadae nchini Uhispania Princess Letizia amejifunguwa mtoto wake wa kwanza.
Mtoto huyo wa kike aliyepewa jina Leonor amezaliwa mapema leo asubuhi.Kuzaliwa kwa msichana katika ukoo wa kifalme kunayapa umuhimu wa dharura mapendekezo ya serikali ya kisoshalisti nchini Uhispania kuifanyia mageuzi katiba ya nchi hiyo ili kuwapa ndugu wa kiume wa kike katika ukoo wa kifalme haki sawa ya kuurithi ufalme.
Leonor yuko nafasi ya pili katika urithi wa Ufalme wa Uhispania akitanguliwa na Felipe na mjukuu wa saba wa Mfalme Juan Carlos na Malkia Sofia.