Madrid: Moto mkubwa huko Uhispania, kwa sehemu, unaanza kudhibitiwa
19 Julai 2005Matangazo
Wazima moto huko Uhispania wamefaulu kwa sehemu kuuzima moto mkubwa ambao uliwauwa wazima moto wa kujitolea 11 na kuharibu sehemu kubwa ya misitu. Moto huo uliosababishwa jumamosi iliopita kutokana na makaa yasiozimwa uzuri baada ya kuchomwa mishikaki na kuzidishwa na pepo kali ulienea katika mkoa wa GUADALAJARA ambao umekumbwa na ukame. Mamia ya watu kutoka vijiji kadhaa na maeeno ya utalii walihamishwa. Ndege zenye maji zilitumiwa leo katika eneo lililokumbwa na balaa hilo. Uhispania hivi sasa iko katikati ya ukame mkubwa kabisa kuwahi kuonekana mnamo miaka 60 iliopita, ujoto ukifikia Digrii 40 za Celcius. Inasekana zaidi ya hektari 8,000 za misitu zimeharibika.