MADRID Wazima moto 11 wafariki dunia nchini Uhispania
18 Julai 2005Matangazo
Wazima moto 11 wamefariki dunia nchini Uhispania wakati walipokuwa wakijaribu kuuzima moto katikati mwa nchi hiyo. Wanaume hao waliojitolea kupambana na moto huo walishindwa kuuzima moto huo ulioharibu sehemu kubwa ya mashamba katika eneo la Guadalajara, mashariki mwa mji mkuu Madrid.
Moto huo ulizuka Jumamosi iliyopita katika mbuga ya wanyama na ukaenea katika maeneo mengi kufuatia upepo mkali. Mikasa mingi ya moto imeripotiwa katika sehemu mbalimbali nchini Uhispania huku nchi hiyo ikikabiliwa na ukame mbaya kabisa tangu miaka ya 1940.