1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maduro aufunga mtandao wa X kwa siku nchini Venezuela

9 Agosti 2024

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameagiza kufungwa kwa mtandao wa kijamii wa X kwa siku 10.

Kombobild I Nicolas Maduro und Elon Musk
Picha: Juan Barreto/Drew Angerer/AFP

Maduro anamshutumu mmilki wa mtandao huo Elon Musk kwa kutumia mtandao huo kueneza chuki baada ya uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata.

Kiongozi huyo pia amewashtumu wapinzani wake wa kisiasa kwa kutumia mtandao huo wa X kuchochea machafuko.

Mwandishi wa habari wa shirika la AP mjini Caracas ameripoti kuwa kufikia jana usiku, mtandao huo ulikuwa haufanyi kazi.

Maduro amesema alitia saini azimio lililoandaliwa na tume ya mawasiliano nchini humo pamoja na kampuni nyengine za mtandao kuufungia mtandao wa X kwa muda wa siku 10.

Mtandao wa X hata hivyo haukujibu mara moja ombi la AP la kutoa maoni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW