1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu bila nguvu za umeme baada ya mashambulizi Urusi

25 Machi 2026

Karibu watu nusu milioni hawana umeme katika eneo la Belgorod nchini Urusi kufuatia mashambulizi ya Ukraine yaliyolenga miundo mbinu ya nishati.

Eneo la Belgorod baada ya shambulizi la Ukraine
Eneo la Belgorod baada ya shambulizi la UkrainePicha: REUTERS

Haya ni kwa mujibu wa gavana wa eneo hilo,Vyacheslav Gladkov.

Gladkov amesema huduma za kupasha joto na majizimeathirika kwa wakaazi wengi pia huku nyuzi joto katika eneo la Belgorod zikitarajiwa kuwa chini ya sifuri katika siku chache zijazo.

Haya yanafanyika wakati ambapo mashambulizi ya Urusi nayo yamesababisha uharibifu katika vituo viwili vya nishati katika eneo la kaskazini mwa Ukraine la Chernihiv.

Kulingana na kampuni ya usambazaji umeme eneo hilo, mashambulizi hayo yamesababisha zaidi ya watu laki mbili kuachwa bila huduma hizo.

Jeshi la Ukraine linasema Urusi imeshambulia kwa droni 147 usiku kucha ambapo 121 kati ya droni hizo zilidunguliwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW