Maelfu ya wafuasi wa siasa za kizelendo waandamana Belgrade
18 Machi 2023Waandamanaji hao wanapinga mpango unaoungwa mkono na mataifa ya magharibi wa kusawazisha mahusiano kati ya Serbia na Kosovo, wanaouona kama utambuzi wa uhuru wa Kosovo, na hivyo usiokubalika. Mpango huo wenye vipengele 11 uliopendekezwa na Umoja wa Ulaya unakusudia kuboresha mahusiano yaliyozorota kati ya Serbia na Kossovo ambayo awali ilikuwa sehemu ya Serbia.
Waandamanaji hao walikusanyika wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa "kataa uvamizi" na "Kosovo haiuzwi".
Soma zaidi Belgrade: Maandamano Serbia kuupinga mpango wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Kosovo
Waliingia mtaani ikiwa ni muda mfupi kabla ya mkutano kati ya Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na waziri mkuu wa Kosovo, Albin Kurti, nchini Macedonia ya Kaskazini. Tangu mwaka 2008, wakati Kosovo ilipotangaza uhuru wake kutoka kwa Serbia, serikali ya Belgrade, ikiungwa mkono na China na Urusi, imekataa kutambua uhuru wa Kosovo.