Maelfu waandamana Brussels kupinga ubanaji matumizi
30 Septemba 2010Matangazo
Brussels ndiko makao makuu ya Umoja wa Ulaya, ambapo polisi walilazimika kuyazingira makao hayo kuzuia waandamanaji.
Inakadiriwa kuwa kiasi ya watu laki moja walishiriki katika maandamano hayo hapo jana.Katibu Mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi barani Ulaya John Monks amesema kuwa wafanyakazi barani Ulaya wamekuwa wahanga wa kuyumba kwa uchumi kulikosababishwa na mabenki pamoja na walanguzi wa fedha.
Wakati huo huo mgomo wa saa 24 umeanza nchini Uhispania na kusababisha usumbufu mkubwa katika sekta ya usafiri wa umma, viwanda vya magari pamoja na sekta nyingine.
Mwandishi:Aboubakary Liongo