1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kaimu Waziri mkuu Sanchez ashutumiwa kuivuruga demokrasria

12 Novemba 2023

Wahispania elfu 80 wamejitokeza kwenye maandamano,Madrid na maelfu katika mji wa Barcelona

Kaimu Waziri mkuu wa Uhispania apingwa na wananchi wake kufuatia mpango wake wa kutaka kuwapa msamaha walioanzisha harakati za kutaka kujitenga kwa jimbo la Catalonia
Maandamano mjini Madrid ya kupinga sera za kaimu waziri mkuu Pedro Sanchez yaliyofanyika Septemba 24Picha: V. Cheretzkij/DW

Maelfu ya watu wameshiriki maandamano ya nchi nzima huko Uhispania, kuipinga mipango ya kaimu waziri mkuu Pedro Sanchez ya kutaka kutoa msamaha kwa wanaopigania kujitenga kwa jimbo la Catalonia,ili aungwe mkono kubakia madarakani kwa muhula mwingine.

Mnamo siku ya Alhamisi serikali ilifikia makubaliano na chama cha wanaopigania kujitenga jimbo hilo cha Junts yanayojumuisha kupitisha sheria inayozusha mvutano,ya kuwapa msamaha wale walioshtakiwa kuhusiana na jaribio la kutaka kutangaza Uhuru wa Catalonia na  kujitenga na Uhispania mwaka 2017.Soma pia:Puigdemont aitaka serikali Uhispania kuheshimu demokrasia

Makubaliano hayo yamewastuwa Wahipania wengi,huku wapinzani wa kaimu Waziri mkuu Sanchez wakimshutumu kwa kuuweka hatarini utawala wa sheria kwa maslahi yake ya kisiasa.

Kiasi waandamanaji elfu 80 walijitokeza katika mji wa Madrid huku maelfu ya wengine wakishiriki maandamano hayo katika miji mingine ya Uhispania,ikiwemo Barcelona.Waandamanaji wanasema Sanchez anaihujumu demokrasia ya taifa hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW