1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Maelfu waandamana kushinikiza mabadiliko ya uongozi Valencia

Angela Mdungu
10 Novemba 2024

Maelfu ya watu wameandamana mjini Valencia nchini Uhispania wakiitaka serikali ya eneo hilo ijiuzulu baada ya mafuriko ya hivi karibuni yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

Maandamano ya raia na mashirika 09.11.24 kupinga namna janga la mafuriko lilivyoshughulikiwa
Waandamanaji dhidi ya uongozi wa Valencia baada ya mafurikoPicha: Ana Beltran/REUTERS

Waandamanaji hao walioingia barabarani Jumamosi  wanapinga namna serikali ilivyoshughulikia maafa hayo, siku kumi na moja baada ya uharibifu mkubwa katika eneo hilo. Maandamano hayo yaliitishwa na mashirika 65 zikiwemo taasisi za kiraia na vyama vya wafanyakazi.

Soma zaidi: Uhispania yatenga zaidi ya $ bil 10 kusaidia waathiriwa mafuriko

Baadhi ya waandamanaji walisikika wakisema "wauwaji wajiuzulu" huku wengine wakiwa na mabango yaliyomtaka kiongozi wa serikali ya eneo hilo, Carlos Mazon ajiuzulu.

Mamlaka zinakadiria kuwa waandamanaji 130,000 walishiriki katika maandamano hayo ya Valencia. Mapema Jumamosi ofisi ya utawala wa Kifalme ya Uhispania ilitangaza kuwa Mfalme Felipe wa sita atatembelea Valencia  ili kufuatilia operesheni za uokoaji na kusafisha maeneo

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW