1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Marekani kupigania uavyaji mimba

John Juma Mhariri: ZAinab Aziz
3 Oktoba 2021

Makumi ya maelfu ya wanawake wameandamana katika zaidi ya miji 600 nchini Marekani kupinga kampeni ya kihafidhina ya kuzuia uavyaji mimba.

USA | Women's March in Washington
Picha: Jose Luis Magana/AP Photo/picture alliance

Mjini Washington takriban waandamanaji 10,000 walijitokeza karibu na ikulu ya rais, White House kabla ya kuelekea katika mahakama ya juu ambayo itatoa uamuzi w amwisho kuhusu suala hilo tete.

Waandamanaji walibeba mabango yenye ujumbe kama ”Iruhusu uavyaji mimba iwe halali kisheria”, ”uavyaji mimba ni suala la Afya na Afya ni haki ya binadamu.”

Vuta nkuvute zisizoisha nchini Marekani kuhusu suala la uavyaji mimba ziligeuka kuwa hata tete zaidi wakati jimbo la Texas lilipopitisha sheria iliyopiga marufuku uavyaji mimba. Sheria hiyo ilianza kutekelezwa Septemba mosi.

Tangu wakati huo shauri nyingi zimewasilishwa mahakamani na bungeni, lakini huu wakati huu ndipo kumekuwa namaandamano makubwa.

Soma pia: Trump afuta misaada kwa wanaotoa mimba

Siku mbili kabla ya mahakama ya juu kuanza vikao, waandaaji w amaandamano hayo wamesema watu waliandamana katika zaidi ya miji 600 na kuongeza kuwa mamia ya maelfu ya watu walishiriki maandamano hayo katika majimbo 50.

Suala la kuruhusu au kutoruhusu uavyaji mimba limekuwa tete kwa muda mrefu nchini Marekani.Picha: Rory Doyle/REUTERS

”Wanawake ni wanadamu, sote ni wanadamu na tunahitaji haki kama wanadamu wote,” amesema Laura Bushwitz, mwanamke mwenye umri wa miaka 66 ambaye ni mwalimu mstaafu wa jimbo la Florida aliyeshiriki maandamano hayo.

”Tunapaswa kuwa huru kujifanyia maamuzi yetu wenyewe kuhusu kile tunataka kufanya na miili yetu,” amesema Michaellyn Martinez ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 70. Alipata mimba akiwa na umri wa miaka 19 kabla ya sheria ya 1973 kabla ya mahakama ya juu ya Marekani kuruhusu uavyaji mimba ikiwa mimba hiyo inahatarisha maisha.

Katika maeneo ya mahakama ya juu, waandamanaji hao walikabiliwa na waandamanaji pinzani waliounga mkono sheria ya kupiga marufuku uavyaji mimba.

Mjini New York, waandamanaji hao walikusanyika katika uwanja wa Manhattan Foley.

Juliettte O'Shea mwenye umri wa miaka 17, aliwashirikisha takriban vijana 30 kutoka shule ya sekondari ya Manhattan.

Waandaaji wa maandamano wasema maandamano yamefanyika katika zaidi ya miji 600Picha: Jeenah Moon/REUTERS

” Tuko hapa kuonyesha kuwa tuko imara na ni kundi la watu ambao walimeungana kutonyamazishwa wakati marufuku ya ajabu dhidi ya utoaji mimba kama ya Texas ikiruhusiwa,” O'Shea aliliambia shirika la habari la AFP.

Tayari mahakama ya juu imekataa kuizuia sheria hiyo ya Texas na pia imekubali kufanyia tathmini sheria ya Mississippi ambayo huenda ikatengeneza nafasi ya kuibatilisha sheria ya Texas iliyotolewa na jaji Roe v Wade.

Hadi sasa ndani ya mwaka huu, majimbo 19 Marekani yameridhia sheria 63 zinazodhibiti huduma za utoaji mimba.

Katika jimbo la Texas ambako gavana mhafidhina Greg Abbott alisaini mswada hu okuwa sheria, mamia ya watu walikusanyika nje ya makao makuu y ajimbo hilo wakiwa na mabango yenye ujumbe, ”Mwili wangu, chaguo langu” na pia ”Muondoe Abbott”.

(AFPE)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW