Maandamano yafanyika mjini Beni
9 Agosti 2019Waandamanaji elfu tano wamefunga barabara za mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na kuchoma moto matairi hapo jana. Waandamanji hao walikuwa wakipinga mauaji yanayofanyika katika eneo hilo ikiwemo vifo sita vilivyotokea katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita kabla ya maandamano hayo.
Kamanda wa jeshi la polisi Kanali Safari Kazingufu amesema maafisa wa polisi waliwatawanya watu na kusafisha barabara kuu za mji huo baada ya waandamaji kuweka vizuizi katika barabara hizo kuanzia saa kumi na mbili na nusu asubuhi.
Maandamano sawa na hayo yalifanyika Jumatano iliyopita, ambapo waandamanaji walitembea umbali wa kilomita 15 kuwasilisha barua katika ofisi ya tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, MONUSCO, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Vikundi kadhaa vyenye silaha likiwemo kundi la Allied Democatic Forces, ADF, pamoja na magenge ya wahalifu yanafanya mashambulizi katika mji huo wa Beni wa jimbo la Kivu Kaskazini, ili kulidhibiti eneo hilo lenye utajiri wa madini.
(afpe)