1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Maelfu waandamana Niger kutaka Ufaransa iondoe vikosi vyake

2 Septemba 2023

Maelfu ya watu wameandamana leo kwenye mji mkuu wa Niger, Niamey, kushinikiza Ufaransa kuondoa vikosi vyake nchini humo kama walivyotakiwa na viongozi wa kijeshi waliofanya mapinduzi mwezi Julai.

Niger Niamey | Demonstranten fordern den französischen Botschafter auf das Land zu verlassen
Tangu mapinduzi yalipotokea, rais wa Niger wamejitokeza kuyaunga mkono na kuipinga Ufaransa.Picha: Mahamadou Hamidou/REUTERS

Waandamanaji walikusanyika nje ya kambi inayowahifadhi wanajeshi wa Ufaransa wakiitikia mwito wa makundi ya kiraia yanayopinga uwepo wa jeshi la mkoloni huyo wa zamani wa Niger. Walibeba mabango yenye ujumbe unaosema "Jeshi la Ufaransa ondokeni nchini mwetu".

Hapo jana kwa mara nyingine watawala wa kijeshi wa Niger waliituhumu Ufaransa "kuingilia bila kificho" masuala ya ndani ya taifa hilo kwa kushinikiza rais aliyepinduliwa arejeshwe madarakani.

Rais Mohammed Bazoum, mshirika wa karibu wa Ufaransa ambaye kuchaguliwa kwake mwaka 2021 kulileta matumaini ya uthabiti nchini Niger, aliondolewa madarakani kwa nguvu mnamo Julai 26.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW