1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Peru kuipinga serikali

Hawa Bihoga
20 Januari 2023

Makabiliano makali yameshuhudiwa baina ya polisi na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu wa Peru Lima, ambapo idadi ya vifo imeshuhudiwa kuongezeka kutokana na ghasia hizo hadi kufikia 45.

Peru I Peruaner protestieren und fordern den Rücktritt von Präsident Boluarte
Picha: Klebher Vasquez/AA/picture alliance

Waandamanaji wanashinikiza rais wa taifa hilo la Amerika ya kusini ajiuzulu na kuitishwa kwa uchaguzi mwaka huu 2023.

Waandamanaji wanaotaka serikali iliopo mamalakani kujiuzulu waliwarushia mawe na chupa maafisa wa kutuliza ghasia wakati maandamano hayo yakisambaa katika miji mingine nchini humo.

Polisi imelazika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waanamanaji.

Peru imekubwa na maandamano tangu kuondolewa madarakanikwa mtangulizi wa Rais wa sasa Dina Boluarte, Pedro Castillo mapema mwezi Decemba hatua iliozusha ghasia kubwa nchini humo hasa katika maeneo ya kusini na mashariki.

Katika mji wa kusini wa Arequipa, waandamanaji takriban 1,000 walijaribu kuvamia uwanja wa ndege siku ya Alkhamis, lakini walizuiliwa na polisi waliofyatua mabomu ya machozi.

Soma pia:Rais aliyeondolewa madarakani nchini Peru awekwa kizuizini

Waandamanaji hao ambao wamesambaa katika mji mkuu wakitokea kwenye mikoa mbalimbali walilenga kufika kwenye ikulu yenye ulinzi mkaali hapo jana Alkhamis.

Mmoja wa waandamanaji amekaririwa na vyombo vya habari akisema maandamano hayo yanalenga kupigania haki yao ya kidemocrasia.

Amsema miongoni mwa madai yao wanataka kuitishwa upya kwa uchaguzi na kufutiliwambali kwa bunge.

"Tunachohitaji ni kujiuzulu kwa Rais Dina Boluarte" alisema huku akiwa kashika chupa ya maji ili kukabiliana na athari za gesi ya machozi zinazofyatuliwa na polisi.

Ameongeza kwamba "tunataka kufutwa kwa bunge na kuitishwa kwa uchaguzi mwingine 2023."

Idadi ya vifo yafikia 45 nchi nzima

Polisi wakijiandaa kuwakabili waandamanaji PeruPicha: Juan Carlos Cisneros/AFP

Waandamanji katika mji mkuu wameendelea kuweka shinikizo kwa serikali kuu na kukaidi hali ya hatari iliotangazwa na mamalaka ili kuleta utulivu.

Mkuu wa polisi Victor Zanabria amesema wamechukua hatua kadhaa za kiusalama ili kudhibiti maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na kusambaza maafisa 11,800,  zaidi ya magari 120 na magari 49 ya kijeshi.

Soma pia:Bunge la Peru lamwapisha Rais mpya Dina Boluarte

Mchunguzi wa masuala ya Haki za Binadamu wa Peru ametangaza kifo cha mtu mmoja katika mji wa Arequipa na kuongezeka kwa vifo vya watu wawili kutokana na ghasia ya siku ya Jumatano hatua iliofikisha jumla ya vifo 45, nchini kote kufuatia maandamano hayo.

Boluarte:Nani anafadhili maandamano haya?

Akizungumza kupitia televisheni ya taifa rais Boluarte amehoji ni nani ambae yupo nyuma ya vuguvugu hilo ambalo limegharimu maisha ya wananchi wasio na hatia.

Rais wa Peru Dina BoluartePicha: Cris Bouroncle/AFP/Getty Images

Katika hotuba yake iliofuatiliwa kwa ukaribu na waandamanaji wakitaka kujua kama wamejibu hoja zao amesema hakuna faida katika maandamano hayo yaliosababisha machafuko na kuyataja ni kinyume cha sheria.

"Kwa wale wanaoandamana kila siku ni nani anaewafadhili?" Alihoji katika sehemu ya hotuba yake.

Soma pia:Rais wa Peru aondolewa madarakani

"Mnadai madai nje ya utawala wa sheria mkitaka kuiondoa serikali."

Alisema rais huyo na kuwataka wafanye kazi ili kuleta ustawi katika familia zao na kuachana na maandamano aliyoyataja hayana faida kwa jamii wala taifa hilo.

Boluarte alikuwa mgombea mwenza wa zamani na makamu wa rais wa Castillo kabla ya kuchukua wadhifa wa urais,hatua ambayo haikubaliki kwa wafuasi wa mtangulizi wake na hata kumshutumu kama "msaliti".

Bi Boluarte, mwanasheria mwenye umri wa miaka 60, ni mwanamke wa kwanza kufikia ngazi ya urais nchini Peru,ikiwa tangu ipate uhuru wake zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Amesema anaunga mkono uchaguzi wa rais na wabunge kufanyika 2024, wakati hapo awali ulipangwa 2026.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW