1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Ujerumani kupinga ubaguzi

8 Juni 2020

George Floyd hakuwa mtu mweusi wa kwanza kuuliwa na polisi weupe nchini Marekani lakini kifo chake kimetifua maandamano makubwa ya kupinga kuuliwa kwake ndani na nje ya Marekani.

Deutschland Black Live Matter Proteste in Köln
Picha: DW/S. Bonney-Cox

Maalfu kwa maalfu kwenye miji mbalimbali ya Marekani na duniani kote walijitokeza mwishoni mwa wiki iliypoita kupinga mauaji ya George Floyd yanayoonyesha kuwemo kwa mfumo wa kibaguzi ndani ya polisi ya Marekani.

Mwenyekiti wa jumuiya ya watu weusi nchini Ujerumani. ISD,Tahir Della ameeleza kuwa ameshangazwa juu ya harakati zinazoendelea duniani kote kupinga mauaji hayo. Mwenyekiti huyo amesema ametiwa moyo kuona kwamba watu wengi duniani kote wanaendelea kushiriki katika harakati za kupinga mauaji ya George Floyd. Ameeleza kuwa watu duniani kote sasa wanazungumzia juu ya udhalimu wa mfumo wa ubaguzi.

Baadhi ya waandamanaji waliobeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kukemea ubaguzi wa rangi na mauaji ya watu weusiPicha: DW/S. Bonney-Cox

Bwana Tahir Della amesema jumuiya yake haijawahi kuulizwa maswali mengi na vyombo vya habari juu ya suala hilo kama ilivyo hivi sasa.

Hali ya nchini Ujerumani

Kuhusu hali ya Ujerumani mwenyekiti huyo amesema mengi yamefanyika kwa ajili ya watu weusi wapatao milioni moja nchini hapa.

Amesema hapa nchini Ujerumani wapo wabunge weusi na pia wapo kwenye bunge la Ulaya. Hata hivyo idadi yao ni ndogo.

Bwana Tahir Della ameeleza kwamba mtu anaweza kusema ubaguzzi umetendeka pale ambapo nia ya kutenda hivyo inaonekana dhahiri.

Baadhi ya waandamanaji Bonn wanaopinga ubaguzi wa rangiPicha: DW/E. Venkina

Kuhusu George Floyd mwenyekiti huyo wa jumuiya ya watu weusi nchini Ujerumani ameeleza kwamba maandamano makubwa ya kupinga kifo chake yametokana na sababu kadhaa.

Tahir Della amesema mitandao ya kijamii imechangia lakini pia huduma duni za afya kwa watu weusi nchini Marekani zimechochea harakati za upinzani dhidi ya ubaguzi.

Mwenyekiti wa jumuiya watu weusi nchini Ujerumani Tahir Della katika ufafanuzi juu ya suala la ubaguzi amesema nchi nyingine zimepiga hatua ndefu zaidi ukilinganisha na Ujerumani. 

Ametoa mfano wa kuuliwa kwa watu wapatao wanane katika mji wa Hanau mnamo mwezi Februari. Watu hao wote walikuwa na nasaba za uhamiaji.
 

Chanzo: DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW