SiasaAsia
Maelfu wafukuzwa kazi kwa kushiriki mgomo Iran
29 Aprili 2023Matangazo
Afisa mmoja anayesimamia sekta ya mafuta na gesi ya jamhuri ya Kiislamu jana Ijumaa alinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Iran-IRNA akisema wafanyikazi hao katika jimbo la Bushehr wamedai nyongeza ya mishahara na kuboreshwa kwa hali ya malazi na usafiri.Kwa mwaka uliopita wa 2022, Iran ilishuhudia wimbi la migomo ya walimu na madereva wa mabasi ambao walipinga mishahara duni na gharama kubwa za maisha. Tangu mwaka 2018, uchumi wa Iran umekuwa katika athari iliyotokana na vikwazo vya Marekani na kuongezeka zaidi kutokana na mfumuko wa bei, pamoja na kuporomoka kwa sarafu yake, rial dhidi ya dola, ikiwa ni baada ya serikali ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ya kihistoria ya nyuklia ya Tehran.