1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wahamishwa Ufilipino huku kimbunga Man-yi kikikaribia

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2024

Mamlaka nchini Ufilipino zimeamuru meli zote kurejea ufukweni na watu katika maeneo ya pwani kuondoka kwenye makazi yao, wakati kimbunga Man-yi kikikaribia katika taifa hilo.

Kimbunga Usagi kilichoipiga Ufilipino karibuni
Kimbunga Usagi kilichoipiga Ufilipino karibuniPicha: AFP

Mamlaka nchini Ufilipino zimeamuru meli zote kurejea ufukweni na watu katika maeneo ya pwani kuondoka kwenye makazi yao, wakati kimbunga Man-yi kikikaribia katika taifa hilo.

Taifa hilo limekabiliwa na vimbunga vipatavyo vitano katika muda wa wiki tatu zilizopita, na kuwaua watu wasiopungua 163. Hali hiyo imeuchochea Umoja wa Mataifa kuomba msaada wa dola milioni 32.9 kwa maeneo yaliyoathirika zaidi.

Vimbunga viwili vya Trami na Kong-rey vilisababisha mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi, huku watu kadhaa wakiwa bado hawajapatikana, kulingana na taarifa ya serikali.

Soma: Idadi ya waliokufa kufuatia kimbunga Gaemi huko Ufilipino yaongezeka na kufikia 33

Takriban watu 255,000 tayari walikuwa wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao katika mikoa ambayo iko hatarini kuathirika na maporomoko ya ardhi, mafuriko na mawimbi ya dhoruba.

Wanasayansi wameonya kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanaongeza kasi ya vimbunga na kusababisha mvua kubwa, mafuriko na upepo mkali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW