Maelfu wajiunga na maandamano ya kupinga ukatili Marekani
1 Juni 2020Wakati huo huo utawala wa rais Donald Trump uliwaita wanaoongoza maandamano hayo yaliyofanyika katika usiku wa siku tano kuwa ni magaidi wa ndani ya nchi.
Wakati viongozi wa maeneo mbali mbali wakitoa wito kwa raia kuonesha hasira zao kwa njia ya uadilifu kuhusiana na kifo cha mtu mmoja mweusi ambaye hakuwa na silaha, amri ya kutotembea usiku iliwekwa katika miji kama Los Angeles, Houston na Minneapolis , ambayo imekuwa kitovu cha machafuko.
Maandamano yaliyokuwa yakiangaliwa kwa karibu zaidi yalitokea nje ya ofisi za serikali katika mji pacha wa Minneapolis wa St.Paul ambako maelfu kadhaa ya waandamanaji walijikusanya kabla ya kuandamana katika barabara kuu.
"Tuna watoto wa kiume weusi, tuna ndugu weusi , hatutaki wafe. Tumechoka kuona hili likitokea, kizazi hiki hakina hilo, tumechoka kukandamizwa," alisema Muna Abdi, mwanamke mweusi mwenye umri wa miaka 31 ambaye alijiunga na maandamano.
Mamia ya polisi na vikosi vya ulinzi wa taifa viliwekwa kabla ya maandamano licha ya kuwa hakukuwa na ripti za ghasia.
Wakati hakuna hali iliyojirejea la ghasia za kiwango kikubwa ambacho kilitikisa miji katika siku za hivi karibuni, waporaji walivamia maduka na maeneo mbali mbali katika mji wa Philadelphia.
Wachoma moto
Waandamanaji walichoma moto karibu na Ikulu ya Marekani ya White House wakati hali ya wasi wasi na polisi ilipopanda wakati wa siku ya tatu mfululizo ya maandamano ya usiku yaliyofanyika kujibu kifo cha George Floyd mikononi mwa polisi mjini huko Minesota.
Saa moja kabla ya kuanza kwa amri ya kutotembea usiku , polisi walifyatua mabomu kadhaa ya kutoa machozi na mabumu ya kuwatisha waandamanaji katika kundi la waandamanaji wapatao 1,000, kwa kiasi kikubwa wakiwatawanya watu kutoka katika eneo la uwanja wa Lafayette katika barabara kutoka Ikulu ya White House, na kuwatawanya waandamanaji katika mtaa huo.
Waandamanaji walikusanya vibao vya alama za barabarani na vizuwizi vya plastiki na kuchoma moto katikakti ya mtaa H. Baadhi walishusha bendera ya marekani kutoka katika jengo la karibu na kuitupa katika moto.
Rais Trump aliwapongeza wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taifa kwa kusema, "pongezi kwa walinzi wetu wa taifa kwa kazi nzuri waliyofanya mara walipowasili Minneapolis , Minesota, usiku wa jana," alisema hayo katika ukurasa wa Twitter na kuongeza kuwa "wanapaswa kutumika katika majimbo mengine kabla ya kuchelewa !"