1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUingereza

Maelfu wakumbwa na mafuriko ya kimbunga nchini Uingereza

25 Novemba 2024

Hali ya wasiwasi imewakumba wakaazi nchini Uingereza na Wales kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Bert kilichotokea mwishoni mwa wiki.

Uingereza | Kimbunga Bert
Mawimbi makubwa yakipiga fuo za pwani nchini Uingereza kutokana na athari za kimbunga Bert.Picha: Chris J. Ratcliffe/REUTERS

Usafiri wa umma umetatizika pakubwa huku hali ya tahadhari ikitangazwa baada ya kimbunga Bert kuipiga Uingereza na Wales na kuandamana na mvua kubwa na upepo mkali.

Mvua ya kiasi milimita 130 imenyesha katika maeneo mbalimbali na kusababisha mito kufurika na maji kuenea hadi barabarani.

Takriban nyumba 350,000 nchini Uingereza zilitumbukia gizani ingawa huduma ya umeme sasa imerudishwa.

Kampuni ya uchambuzi wa masuala ya anga ya Cirium imesema zaidi ya safari 300 za ndege zimefutwa kutokana na kimbunga Bert.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW