1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya raia wa Kongo waandamana kupinga machafuko

5 Desemba 2022

Maelfu ya ya Wakristo wameingia mitaani kote nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo jana kupinga vurugu zinazoendelea katika mikoa ya mashariki mwa nchi hiyo.

DR Congo Kongolesische Jugendliche schließen sich der Armee an, um Rebellen zu bekämpfen
Picha: Benjamin Kasembe/DW

Maelfu ya Wakristo wameingia mitaani kote nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo jana kupinga vurugu zinazoendelea katika mikoa ya mashariki mwa nchi hiyo huku viongozi wa kanisa wakiituhumu jumuiya ya kimataifa kwa unafiki kuhusiana na madai ya ushiriki wa Rwanda katika mapigano.

Baada ya misa za Jumapili, waumini katika mji mkuu Kinshasa na miji mingine mikubwa waliitikia wito uliotolewa na Baraza la Maaskofu kuandamana dhidi ya mzozo na kundi la waasi wa M23 ambalo Congo inaishutumu Rwanda kuliunga mkono, madai ambayo Rwanda inayakanusha.

Maandamano hayo ya umma ndiyo yalikuwa makubwa zaidi tangu kuongezeka kwa mapigano katika miezi ya karibuni kati ya vikosi vya serikali na M23. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya kiutu, OCHA, mzozo huo umesababisha watu wapatao 390,000 kukosa makazi yao.

Wengi nchini Congo wameyashtumu mataifa ya magharibi kwa miaka kadhaa, kushindwa kuiwajibisha Rwanda kwa madai ya kuchochea hali tete ya usalama mashariki mwa nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW