1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya waandamanaji Korea Kusini wakusanyika Seoul

4 Januari 2025

Maelfu ya waandamanaji nchini Korea Kusini wamekusanyika katika mji mkuu Seol, siku moja baada ya jaribio lililoshindwa la kumkamata rais aliyeondoshwa madarakani na bunge Yoon Suk Yeoul.

Waandamanaji Korea Kusini wakikabiliwa na vikosi vya usalama
Waandamanaji, wanaomuunga mkono na wale wanaompinga Yoon, walikusanyika mbele ya makazi yakePicha: Ahn Young-joon/AP/picture alliance

Maelfu ya waandamanaji, wanaomuunga mkono na wale wanaompinga Yoon, walikusanyika mbele ya makazi yake na kwenye barabara kuu za mjini Seoul, wakizingirwa na mamia ya maafisa wa usalama watiifu kwa rais huyona ambao mpaka sasa wamezuia juhudi za waendesha mashitaka kumkamata.

Wanachama wa jumuiya ya vyama vya wafanyakazi nchini Korea, walijaribu kutembea kuelekea makazi ya Yoon kuandamana dhidi yake, lakini walizuiwa na polisi. Wapelelezi kutoka Ofisi ya Kuchunguza vitendo vya rushwa, wamemuomba waziri wa fedha Choi Sang-mok, ambaye anashikilia wadhifa wa kaimu rais tangu wiki moja iliyopita, kuunga mkono waranti wa kumkamata Yoon.

Mpaka sasa, kitengo cha ulinzi wa rais huyo kimekataa kutoa ushirikiano. Kitengo hicho kimesema maafisa wake wawili wakuu walikataa ombi la kufika mbele ya polisi leo ili kuhojiwa, wakitaja changamoto kubwa ya kumlinda rais huyo anayekabiliwa na mashitaka ya uasi na jinai.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW