Maelfu ya wakimbizi watoroka vita Kongo
24 Juni 2022Wanaokimbilia ndani ya vijiji vinavyodhaniwa kuwa na usalama ikiwemo kijiji cha Rumwangabo mbali kidogo na makao makuu ya wilaya hiyo ambamo mamia wengine wanahangaishwa na ukosefu wa chakula pamoja na maji safi.
soma Amnesty: Raia lazima walindwe Kongo
Mapigano ya hivi karibuni katika vijiji vya Ruvumu ,Chengerero na ambayo yaliendelea hadi jana jioni katika eneo la Nkokwe yamesababisha maelfu ya watu kutoroka makwao ili kutafuta hifadhi katika maeneo tofauti ikiwemo mji wa Goma pamoja na kijiji cha Rumangabo mbali kidogo na makao makuu ya wilaya hiyo ambamo mamia ya wakimbizi hao, baadhi ikiwa ni watoto na wanawake waendelea kuhangaika.
soma Wakuu wa Afrika Mashariki wakubali kupeleka jeshi, DRC
Hali inazidi kuwa mbaya
Hadi sasa, wakimbizi hao wakiwa wameanza kupoteza matumaini ya upatikanaji wa amani kufuatia kasi ya mashambulizi ya kundi la M23 kuendelea kuviteka baadhi ya vijiji wilayani Rutshuru hapa wanasema.
"watoto wetu wana taabika na magonjwa kila wakati, wamekosa hata dawa kwa hiyo tungehitaji mashirika yakiutu yatulee misaada hata amani na usalama ili turudiye nyumbani." alisema mkimbizi mmoja
soma Wakongo na mashirika ya kiraia waliunga mkono jeshi
"hatuna maji wala dawa , hatujamuona yoyote ule anaye wasili hapa kwakutushughulikia nakututolea msaada. " mkimbizi mwengine aliiambia DW.
Katika ripoti iliyochapishwa na mashirika ya haki za binadamu mwanzoni mwa juma hili, imekadiria kuwa watu zaidi ya laki moja wametawanyika kote katika wilaya ya Rutshuru huku elfu 30 kati yao wakiwa wamepiga kambi ndani ya kijiji hiki cha Rumangabo ambamo wasiwasi umeanza pia kutanda baada ya ongezeko hilo la wakimbizi.
Mbali na hayo, watu zaidi ya 20 wameuawa kwa risasi na wengine kukatwa kwa mapanga katika kipindi cha siku tatu ndani ya kijiji cha Ruvumu eneo la Jomba, vifo ambavyo vimeshukiwa kuendeshwa na wapiganaji wa kundi la M23 ambao wamekanusha madai hayo yaliyotolewa kwenye ripoti iliyochapishwa tangu siku ya Jumatano na muungano wa asasi za kiraia wilayani Rutshuru.
Benjamin Kasembe