1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Wanawake wajawazito Haiti hatarini kukosa huduma za afya

Sylvia Mwehozi
9 Machi 2024

Takribani wanawake wajawazito 3,000 nchini Haiti, wanakabiliwa na kitisho cha ukosefu wa huduma za afya, wakati hali ya kibinadamu katika mji mkuu wa Port-au-Prince ikiendelea kuzorota.

Haiti
Wanawake wakikimbia milio ya bunduki HaitiPicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Takribani wanawake wajawazito 3,000 nchini Haiti, wanakabiliwa na kitisho cha ukosefu wa huduma za afya, wakati hali ya kibinadamu katika mji mkuu wa Port-au-Prince ikiendelea kuzorota.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Haiti, imeonya jana kwamba karibu wanawake 450, huenda wakakabiliwa na matatizo ya uzazi ambayo yanatishia maisha ikiwa hawatapokea msaada wa matibabu.

soma: Haiti yarefusha hali ya hatari kwa mwezi mmoja zaidi

Mgogoro wa Haiti umeibua wasiwasi kutoka kwa Marekani ambayo imemtaka waziri mkuu wa nchi hiyo, aliyeko nchi jirani kufanya mageuzi ya haraka ya kisiasa ili kuzuia kuongezeka zaidi kwa ghasia.

Makundi ya wahalifu, ambayo tayari yanadhibiti sehemu kubwa ya mji mkuu pamoja na barabara zinazoelekea katika maeneo mengine ya nchi, yameshambulia miundombinu muhimu katika siku za hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na magereza mawili, na kuruhusu wafungwa zaidi ya 3,000 kutoroka.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW