1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Kagame mgeni rasmi "Rwanda Day" mjini Bonn

5 Oktoba 2019

Maelfu ya Wanyarwanda barani Ulaya wakutana na rais Kagame mjini Bonn

Bonn Ruanda Day Präsident Paul Kagame
Picha: DW/I. Mugabi

Rais Paul Kagame wa Rwanda (05.10.2019 amewahutubia raia wa Rwanda waishio barani Ulaya na kugusia masuala kadhaa muhimu ambayo yanalihusu taifa lake. Kagame akiwa na mkewe Janeth Kagame alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kila mwaka iitwayo "Rwanda Day" ambayo safari hii imefanyika katika jiji la Bonn nchini Ujerumani.

Katika hafla hiyo ambayo ilianza rasmi alasiri na kuhimitishwa saa 2:30 usiku kwa muda wa  Ulaya ya Kati, Rais Kagame amejibu maswali mbalimbali ya raia wa Rwanda walihudhuria ambapo, hoja zilikuwa nyingi na ikamlazimu rais kuwataka raia hao watumia majukwaa mengine maaalum ya kufikisha kero zao ni si kusubiri Siku ya Rwanda, ambayo inatoa fursa finyu.

Misururu ya raia wa Rwanda katika mkutano wa Siku ya RwandaPicha: DW/K. Tiassou

Siku ya Rwanda inahusu masuala ya jamii ya Wanyarwanda, serikali yao, lakini pia kuhusu wafanyabiashara ambao wako Rwanda na Ulaya, hivyo wamekutana kuangalia jinsi watu wa Ulaya wanavyoweza kuisaidia Rwanda katika masuala mbalimbali ya miradi ya maendeleo.

Mapema Asubuhi kwa kutumia usafiri wa mabasi, maerefu ya watu, wengi wao wametokea mataifa ya Uingereza, Uholanzi, Ubelgiji, Uswisi, Austria na maeneo mengini ya Ulaya waliwasili. Kagame anaonekana kama mshirika wa kuaminika wa kimataifa katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na kimaendeleo, ingawa anajulikana pia katika dhamira yake na msimamo mkali kuhusu masuala ya Rwanda. Mkutano huu wa Bonn, unafanyika kukiwa na ulinzi mkali wa polisi na hata kutoka kwa upande wa maafisa wa usalama wa Rwanda