1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya watoto waachwa bila ya makazi mashariki mwa DRC

31 Julai 2022

Maefu ya watoto wameachwa bila ya makazi huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo jeshi la taifa linakabiliana na waasi wa M23.

Kongo Flüchtlingslager in Goma
Picha: AP

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema zaidi ya watu 190,000 nusu yao ikiwa ni watoto, wamelazimishwa kuvikimbia vijiji vyao katika maeneo ya Rutshuru na Nyiragongo.

Akizungumza baada ya ziara yake ya majimbo ya Rutshuru na Kivu ya Kaskazini, mwakilishi mkazi wa UNICEF kwa DRC, Grant Leaity amesema maelfu ya watoto wapo katika mazingira hatarishi na ukata wa kupata mahitaji ya msingi katika kunusuru maisha yao.

Mwakilishi wa UNICEF kwa DRC, Grant Leaity asema hali uenda ikawa mbaya zaidi.

Wakimbizi watoto mjini Goma huko DRCPicha: AP

Mwakilishi huyo alikutaa na baadhi ya walioachwa bila ya makazi katika eneo la Rutshuru amesema hali hiyo uenda ikaendelea katika kipindi hiki ambacho waathirika wanaogopa kurjea nyumbani. Aidha amesema misaada ya kiutu imekuwa midogo katika kipidi hiki ambacho inahitajika zaidi.

Katika eneo la Karenga idadi ya watu wasio makazi imekuwa kubwa kuliko imekuwa mara mbili ya jumla ya idadi ya wakazi halisi wa eneo hilo. UNICEF imesema familia za wasio na makazi na zile zinaziwapa hifadhi zipo katika udharura wa kuhitaji chakula, vifaa vya nyumbani, afya na maji na usafi.

Baadhi ya raia wa DRC wanaonekana kurejea katika mazingira ya vijiji vyenye machafuko.

Shirika hilo limeonya kuwa kutokana na hali ya kutokwepo kwa msaada baadhi ya watu wanalazimika kurejea katika vijiji vyao ambavyo amani hakuna. Mwakilishi Leaity amesema "ni muhimu kuchukua hatua sasa ili kuzuia ongezeko kubwa la visa vya watoto wanaougua utapiamlo mkali."

Kundi la M23, lenye wanachama wengi wa jamii ya Watutsi ambalo lilisambaratishwa 2013, hivi sasa limerejea tena na kudaiwa kushambulia jeshi la DRC na walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kadhalika na kufanikiwa kuyadhibiti maeneo kadhaa. Serikali ya Congo imekuwa ikiishutumu Rwanda, madai ambayo Rwanda imeyakanusha.

Chanzo: AFP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW