1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Maelfu ya watu waandamana Georgia kupinga uchaguzi wa bunge

29 Oktoba 2024

Makumi kwa maelfu ya watu wameandamana jana usiku katika mji mkuu wa Georgia Tbilisi kupinga ushindi wa chama tawala cha Georgian Dream katika uchaguzi wa bunge.

Maandamano Georgia kupinga matokeo ya uchaguzi wa bunge
Waandamanaji nchini Georgia wanadai uchaguzi wa bunge uliingiliwa na Urusi Picha: Alexander Patrin/ITAR-TASS/IMAGO Images

Hayo ni wakati upinzani ukitoa miito ya kurudiwa uchaguzi huo chini ya uangalizi wa kimataifa. Rais anayeegemea nchi za Magharibi, Salome Zourabichvili, aliwahutubia waandamanaji, huku watu wakipeperusha bendera za Ulaya na Georgia mbele ya bunge.

Rais alisema hatoyatambua matokeo ya uchaguzi wa Jumamosi kwa sababu yalichakachuliwa na kuwa dosari nyingi zilitokana na uingiliaji wa Urusi. Licha ya ushahidi wa kutosha wa dosari, tume ya uchaguzi ya Georgia ilikitangaza chama tawala cha kihafidhina cha siasa za kizalendo Georgian Dream kuwa mshindi kwa asilimia 54 ya kura.

Soma pia: Upinzani nchini Georgia waitisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa bunge

Miungano ya upInzani inayoegemea Ulaya ilipata asilimia 11 ya kura. Urusi imesema haikuingilia katika uchaguzi huo. Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema madai hayo hayana ushahidi. Kremlin inautuhumu upinzani kujaribu kuidhoofisha nchi na kusema uingiliaji wowote hakutoka "upande wa Urusi."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW